Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), inapitia upya sera ya mashirika hayo ili kuyabana yasiyofuata sheria.
Akizungumza leo Julai 11 katika mkutano wa kuziwezesha NGO jijini Dar es salaam, Naibu Mkurugenzi wa usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali, Baraka Leonard amesema maboresho hayo yanafanywa na mashirika hayo.
"Kwa sababu hata kwenye familia kuna watoto watukutu. Lakini katika hatua hii, tutaweka masharti ili kuwabana watoto watukutu," amesema Baraka.
Awali, Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya serikali (Nacongo), Ismail Suleiman amesema sera iliyopo sasa ni ya mwaka 2001 hivyo inatakiwa kuboreshwa ili kwenda na wakati.
Amesema lengo la mkutano huo ni kuwaandaa wataalamu 30 kwa ajili ya kwenda mikoani kukusanya maoni ya wadau.