Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka (2001) inaweka msingi wa uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi wa Mashirika hayo kwa kutoa maana ya Shirika Lisilo la Kiserikali, kuainisha vyombo vya usimamizi vya Mashirika na kuweka utaratibu wa kusajili Mashirika. Sera hii ndiyo msingi wa kutungwa kwa Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24/2002.