Serikali yapitia upya sera ili kuzibana NGO’s zisizofuata sheria

Dar es Salaam. Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), inapitia upya sera ya mashirika hayo ili kuyabana yasiyofuata sheria.

Naibu Mkurugenzi wa usajili wa NGOs' Baraka Leonard akitoa neno

Akizungumza leo Julai 11 katika mkutano wa kuziwezesha NGO jijini Dar es salaam, Naibu Mkurugenzi wa usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali, Baraka Leonard amesema maboresho hayo yanafanywa na mashirika hayo.

“Kwa sababu hata kwenye familia kuna watoto watukutu. Lakini katika hatua hii, tutaweka masharti ili kuwabana watoto watukutu,” amesema Baraka.

Awali, Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya serikali (Nacongo), Ismail Suleiman amesema sera iliyopo sasa ni ya mwaka 2001 hivyo inatakiwa kuboreshwa ili kwenda na wakati.

Amesema lengo la mkutano huo ni kuwaandaa wataalamu 30 kwa ajili ya kwenda mikoani kukusanya maoni ya wadau.

  • Google+
  • PrintFriendly

National Council of NGOs, Tanzania

National Council of NGOs
P.O.BOX 34163,Dar es Salaam.
6Kiko Avenue(3rd floor) Mikochen A
Tel.: 022 277 2402
Mobile: 0694058019
Email: .(JavaScript must be enabled to view this email address)

 

Partners

    This Section is Being Updated!